Isaiah 27:2-6

2 aKatika siku ile: “Imbeni kuhusu shamba la mizabibu lililozaa:

3 bMimi, Bwana, ninalitunza,
nalinyweshea maji mfululizo.
Ninalichunga usiku na mchana
ili mtu yeyote asije akalidhuru.

4 cMimi sijakasirika.
Licha pangekuwepo michongoma na miiba kunikabili!
Ningepambana dhidi yake katika vita,
ningeliichoma moto yote.

5 dAu niwaache waje kwangu kwa ajili ya kupata kimbilio,
wao na wafanye amani nami,
naam, wafanye amani nami.”


6 eKatika siku zijazo, Yakobo atatia mizizi,
Israeli atatoa chipukizi na kuchanua maua,
naye atajaza ulimwengu wote kwa matunda.

Copyright information for SwhKC